Sunday, May 27

Mmeshafaya homework?


Kama kawaida...Bibi to the rescue! (what will I do without you mama?) Namba 3 ilinishinda mie, afu nna hasira za karibu, ikabidi bibi achukue usukani, waende taratibu hadi kieleweke!
Kwa wale wenye schoolers wawe wa vidudu, primary au sekondari nawakumbusha tu kufanya homework, kama ulisahau...
Lunch itakua ishaliwa, mdau ameshashiba, kama ilisahaulika, basi homework ifanyike, ili kesho asitoe hadithi ya mbuzi kala daftari langu kwa ticha!

Hizi homework si za watoto tu, na wazazi tunahusika...fanya naye, hata kama wa sekondari jihusishe kwenye anoyojifunza, ili ujue ana uelewa gani...hata kama una elimu ndogo kuliko yeye, ukisoma hapa basi si unajua kusoma, basi soma naye somo la Kiswahili, ukiwa artistic kama kina mie, basi msaidie hata kupaka rangi...

Sio unamwachia anko, anti, sometimes dada kila siku...au mama kumwachia baba, or baba kumwachia mama kila siku--hafai. Afu akipata zero unashangaa, sasa kama ulikua hufatilii unaishia kujisifu tu "mwanangu ana akili, anajua bilinganya kwa kizungu, yaani full english, kiswahili hata hajui!" utajuaje            kuwa anaelekea kwenye zero???

Swali ni mmeshafanya homework leo? Kama bado FANYA sasa!



Unajua cartoon zinazomfaa mtoto wako?

Watoto wengi wanapenda sana katuni.
Hili liko wazi na wala halipingiki. 
Lakini Mzazi hivi unafahamu kwamba sio kila katuni ni ya 
kuangaliwa na mtoto wa umri wa mwanao?


bofya hapo kushoto tujuzane....



Saturday, May 26

J&J wanawapa Hi!

Wadau wenzenu Jasmine na kaka yake Japhary wanawapa hi. 

 Cute J mdogo.

Luvly J mdogo na J mkubwa.

Friday, May 25

Just cuuuute...

Anaitwa Jill, tulimuona kwenye picha za Mother's Day na mama yake Christina... 


 this girl is just toooo cuuuute!

Thursday, May 24

Hausigeli anayedaiwa kumuua mtoto anusurika kifo

 
Mwezi Machi mwaka huu, habari ya hausigel kumuua mtoto wa bosi wake
  ilitikisa jiji la Dar na nchi nzima kwa ujumla.
Wazazi tunaowategemea hawa wasaidizi 
wetu wa nyumbani tulipatwa na hofu, tukapigwa na bumbuwazi 
na kupata mfadhaiko
 baada ya kusikia habari katika vyombo vya habari juu ya hausigeli 
aliyedaiwa kumuua mtoto huyo wa miezi saba aliyeitwa Angel.
Jana huyo dada kakamatwa na kidogo apigwe ila wasamaria wakamuepushia kifo, na kumuepushia balaa zaidi mama wa mtoto (maana naye angesababisha kifo cha dada huyo kwa hasira ingekua mbaya kwake) na amefikishwa polisi.
Kwa habari kamili gonga hapa  HABARI LEO

Unamwekea mwanao akiba?

Hebu tujuzane, Hivi umeshawahi kufikiria kumwekea mwanao akiba?
Je unajua umuhimu wa kumuwekea mwanao akiba?
Ni wazazi wangapi wamewawekea watoto wao akiba aidha benki, mchagoni au kwenye kibubu?
Inawezekana hufahamu akiba ni kitu gani hebu tujuzane kwanza maana ya akiba.
Akiba: Ni kiwango fulani cha pesa kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Haijalishi akiba inawekwa wapi, popote pale ni akiba.
Dunia ya leo hatujui kesho yetu. Wazazi ni muhimu kuwawekea watoto wetu akiba. Ebu imagine umfungulie mwanao akaunti ya benki halafu kwa kila mwezi umwekee 20,000 tu. Je akifika umri wa shule utakosa ada ya kumlipia shule nzuri? Kama unaona ni ngumu kwenda kupanga foleni benki kila mwezi benki unaweza kuweka standing order ili hela itoke kwenye account yako iende kwenye akaunti yake moja kwa moja.
Inawezekana huna mshahara ila una vitega uchumi vingine. Je umejiandaaje kwa ajili ya baadaye ya mtoto wako?
Mfano una nyumba tatu umepangisha, moja kati ya hizo unaweza ukatumia kodi yake kwa ajili ya kusave kwenye akaunti za watoto wako.
Tujijengee utamaduni wa kuwawekea akiba watoto wetu. Kesho yetu hatujui itakuwaje, tutumie pesa vizuri huku tukiwafikiria watoto wetu kesho yao. Kama tunawapenda watoto wetu tuwe na utaratibu wa kuwawekea akiba. 
Wahenga walisema Akiba Haiozi.

Je umemwekea mwanao akiba wapi? Ebu washirikishe wazazi wenzako katika hili.


Nimeona comment ya mdau anavyomaliza akiba ya mtoto - Unawezaje kuhakikisha huvunji kibubu cha mtoto? - tuongee wiki ijayo...

Wednesday, May 23

Dada amlisha damu ya hedhi mtoto???


Siku hizi karibia nyumba nyingi sana zina house girls na hawa huwa muhimu sana katika kutuangalizia nyumba zetu na watoto wetu haswa pale tunapokuwa hatupo nyumbani, na siku hizi nyumba nyingi huwa na house girl wawili yani mmoja kwa ajili ya watoto na mwengine kwa ajili ya nyumba kwa ujumla, sasa basi huyu house girl wako ulimpataje? unapajuwa kwao? ama ndio wale tu tunaoletewa kwa kupigiwa simu na sisi kwavile tunawahitaji sana tunawakaribisha nyumbani kwetu bila hata kutaka kuwajuwa kwa undani sikia mkasa huu..


Kuna familia moja ndio kwanza walikuwa wameoana na wanamtoto mmoja hii familia ilihitaji msichana wa kazi kwasababu wote walikuwa ni wafanyakazi ili aweze kukaa na mtoto, basi tafuta huku na kule siku moja yule mama akaambiwa kunamsichana wa kazi kijijini singida tuma hela apakiwe kwenye gari aje, basi kwavile yule mama naye alikuwa na shida wa msichana kweli kwa haraka bila kuchelewa akatuma hela yule msichana akapakiwa kwenye basi baada ya siku tatu akawasili dar.

Yule mama akampokea na kukaa naye vizuri kama ndugu yake yani hakuna ambalo jema hakumfanyia yule msichana maana yule dada kweli alikuwa anajituma sana katika kazi zake yani watu walioingia ile nyumba walimtamani sana yule dada, miezi sita ikapita yule dada wala hakubadilika katika utendaji wake wa kazi.

Basi siku moja hivi yule mtoto wa mama mwenye nyumba akaumwa ghafla wakamkimbiza hospital, walipomfanyia uchunguzi wakabaini alikuwa ana food poison ndio maana alikuwa anaumwa sana mpaka kuishiwa nguvu maana anatapika sana pia, basi akapata matibabu na kupona lakini cha kushangaza yule mtoto alikuwa akipata hayo matatizo kila mwezi mara kwa mara, wazazi wake wakiwa hawaelewi ni kwa nini.


Tuesday, May 22

Best wishes Naomi

 
Mdau Naomi Lugoe yuko kwenye hatua za mwishomwisho kutuletea malaika...

...hizi picha nimezipiga last week, though yuko mwishoni, bado ana nguvu na uchangamfu wake kama kawaida. 
Mama na Mwana wish you all the best. xoxo.

Thursday, May 17

Bosi anapomuunguza mtoto wa 'hausigeli' inakuaje?



Mara nyingi tunasikia stori za wasichana wa ndani aka hausegirls aka dada wakiwafanyia vitu vya kikatili watoto wa waajiri wao. Sasa hii ni kinyume, mama mwajiri amemchoma kwa maji ya moto mtoto wa dada.
Anadai alikua analipiza kwa dada, kwani alishawahi kumchoma mwanae pia. Mtoto huyo wa miaka miwili amelazwa Muhimbili.
Ilikuaje, zama ndani zaidi...

Happy Birthday Melissa

Leo ametimiza miaka minne.

                           Melissa Mungu akulinde na kukuza…Tunakupenda sana

Says…….
Mamy Siyabonga

Wednesday, May 16

Kindumbwendumbwe...



Gud mamaz, 


Kuna matukio mbalimbali yanayotokea mitaani  kwetu ambayo ni unyanyasaji wa watoto. Lakini labda huenda wanaoyafanya hawajui kama huo ni unyanyasaji.  

 Mamaz mnazungumziaje swala la mtoto  kufanyiwa KINDUMBWENDUMBWE,
 eti kwa kuwa amekojoa Kitandani?



Kwa msiojua;
Kindumbwendumbwe
Ni kitendo cha kumzungusha mtoto mtaa mzima,
akiwa na nguo zake alizozikojolea, 
na mashuka yakiwemo huku watoto wengine (na watu wazima wakati mwingine) 
wakimfata kwa nyuma wakimzomea na kumwimbia.


        "Kindumbwendumbwe! Chalia! Kikojozi kakojoa! Na nguo kazitia moto”


Hii kitu ina madhara kwa mtoto na inaweza kumjengea mtoto kutokujiamini,
 kukosa raha na saa nyingine inaweza 
kumfanya mtoto kuwa mkatili.


Ukiwa kama mzazi unakichukuliaje kindumbwendumbwe? 




Usafi wa meno ya mtoto



Mtoto anapaswa kuanza kusafishwa meno pale tu baada ya kuota. 

Usiulize vijino viwili mswaki wa nini...mswaki lazima hata kwa kijino kimoja!

Wazazi wengi tunajisahau sana katika hili hivyo kuyafanya meno ya 
watoto wetu kuwa machafu na kukosa ung’aavu.


Mtoto anapaswa kupigishwa mswaki kwa kutumia dawa ya meno ya watoto.
 



 Dawa za watoto

Dawa za meno za watoto zipo nyingi sana na za aina mbalimbali. Tofauti ya dawa hizi na zile za watu wakubwa hizi hazina madhara hata kama mtoto ataimeza kwa kuwa haina fluoride.

Pia mswaki wa mtoto utumike ili kuepusha kumuumiza kwani umetengenezwa laini kulinganisha na ugumu wa fizi zake.



Miswaki ya watoto 

Tembelea Supermarkets kujichagulia dawa ya meno na miswaki ya mwanao.

Kwa taarifa zaidi juu ya usafi wa meno ya mtoto ingia HAPA



 

Majina 10 bora ya 2011 Marekani


Haya ni majina kumi yaliyotumika sana kwa wamarekani  kuwapa watoto wao kwa mwaka jana .

Ya Kiume:
1. Jacob
2. Mason
3. William
4. Jayden
5. Noah
6. Michael
7. Ethan
8. Alexander
9. Aiden
10. Daniel


Ya Kike:
1. Sophia
2. Isabella
3. Emma
4. Olivia
5. Ava
6. Emily
7. Abigail
8. Madison
9. Mia
10. Chloe



Kuona majina yaliyoongoza 2010 BOFYA HAPA!

Tuesday, May 15

Feza's Mother's Day celebration

 Wamama wa watoto wanaosoma  Feza Nursery School tulialikwa Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya Mother's Day ambayo waalimu walituandalia.
Tulikaribishwa na mkuu wa Feza Nursery School. Ms Bushra...

...wamama tulikua wengi wa kutosha... 

 KGI, kina Xchyler, ndo walianza kwa kutuimbia...very touching song about mama...

...hapa wanasema I love you... 




Hawa ni KG III...nalifanya kama poem about mama...hapa wanasema, whatever I give you, you give it back much much more...sikumbuki maneno yote, ila maana ni kama hiyo...pia ilikua bomba sana! 

Happy birthday Glory


Mdau Glory, binti wa Jacqueline Moshi, ametimiza miaka minne (4) leo.
Mama na Mwana inamtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa, Mungu amwongoze maishani! 

Monday, May 14

Umenyonyesha muda gani? Are you a mom enough?

Hii nni cover ya time iliyoleta utata sana huko kwa wenzetu...
Kwanza ni hiyo headline ya Are you a mom enough?
na kwa wenzetu huko ambako kunyonyesha hadharani ni issue ya kuweka picha ya mtoto anayonya kama hivi pia ni balaa.
Ila kubwa zaidi ya yyote ni kwamba watoto waachishe kunyonya lini? 
Huyu mtoto anakaribia miaka minne.

Nimenyonyesha watoto wangu, wa kwanza miezi sita na wa pili miezi saba tu, am I a less mom kuliko aliyenyonyesha mwaka mzima au miaka miwili?
Na asiyenyonyesha kabisa, je yeye ni less mom kuliko walionyonyesha? 
Mama, baba tupia comment yako hapo chini!

Article yenyewe kuhusu njadala wa hii issue hii HAPA!

Sunday, May 13

Happy Mother's Day wadau...


Esther na mwanae anitwa Newton Newton. Hawa ni wadau wa Morogoro.

Christina & Jill

 Happyness & Aaliyah

Fatma & Nasreen

Rebecca & Rachel


Rachel & Risper

Happy Mother's Day wadau wote..
Love, Jiang.

Friday, May 11

Bonge la b'day bash for Risper

...huyu ndo birthday gal mwenyewe, anaitwa Risper...she is now 3years. 
Birthday yake ilikua tarehe 6 May. Hongera sana cutieee. 

...Risper na mom, Rachel... beauty is in the genes jamani! 

...tamtam ya mdoli... 


...kata-keki-tuleee...nani asiyependa muda huu? 






baada ya marafiki,  then kwa mama

Thursday, May 10

Lunch njema wadau...


....nimempendaje??? mwili unaonyesha hataki utani na mlo, chezea kingine si mlo wake... mtoto wa hivi raha sana, poleni kwa wenye wadau wanaoringa kula, mie included kwa X mkubwa!

Happy birthday Justus



Mdau Justus ametimiza miaka sita (6) jana tarehe 9, May. 
Hapa anamlisha mamie wake Alice Ngubwene


...Tam tam... 



Birthday boy aki-kata-keki-tule shuleni kwake, Filbert Bayi School, Kimara