Thursday, March 4

Msaada tutani: Boyfriend kakataa mimba!

Hello Jiang,
kwanza nakupa hongera kwa kazi unayofanya nafikiri kuwa na kazi ya ofisi,mama wa mtoto na kublog si mchezo,endeleza kasi nzuri.
mimi ni mdada wa miaka 27,pia samahani kama nitakuwa nimekusumbua lakini katika kuangalia nimeona wewe uko very positive na maisha hasa kuhusu watoto,nimejifunza kutotafuta ushauri kwa mtu ambaye ni negative mara nyingi,
sasa tatizo langu ni hili imetokea katika maisha yangu ya mahusiano nimekuatana na mtu tukapendana kwa muda ambao nakiri sio mrefu wa kutosha tukafanya zile habari za wapendanao lakini ile siku tu kumbe haikuwa salama kwangu nikapata ujauzito,kweli nilikosea kukubali kufanya mambo ayo in the first place mbaya
zaidi sikutumia kinga kweli hapo najua nimekosea hasa usinishutumu nimeshakiri
Shida inakuja baada ya kumuambia huyo boyfriend akasema hana muda  wa   kulea  mtoto sasa hivi kwanza anataka kwenda nje ya nchi mwezi wa tano(mambo yakienda sawa wangu atazaliwa mwezi wa sita)  kwa  sababu  hiyo niitoe hiyo mimba, nijibu tu kwamba lakini mbona watu wanalea watoto zao wakiwa mbali akageuka ooh umenitegeshea kulala na wewe siku moja tu umeingia mimba kwani hukujua kama ni siku ya hatari? nikamjibu tu unakumbuka nilivyokulazimisha tutumie kinga ukakataa? hakukubali ukweli, basi uhusiano ukaanza kuyumbia pale siku moja akawa nje ya dar nikaamua tu kutoka moyoni nikijua atakuwa na msimamo tofauti,najuta hata kwanini niliwasiliana naye siku hiyo,akaniuliza enhee vipi hiyo mimba umeishaitoa mimi nikamuambia bado, akauliza kwani ina muda gani nikamuambia ndio inamaliza mwezi inaelekea mwezi wa pili,akaniambia sasa kinashindikana nini si tutoe tu bado ndogo hiyo,nikamwambia siko tayari mi naona kwa sasa sina kipingamizi nitamlea tu huyu mtoto,(nilishawahi kutoa mimba kabla,mungu anisamehe nikaapa sitarudia tena maishani mwangu)
Basi ndio akaniambia unajua sio vizuri kuzaa watoto wawili wakati hujaoa                        na nilishakuambia mi nina mtoto wa miaka miwili sasa itakuwaje mi nikamuambia sio shida nitaficha tu kwa watu kwamba sitataja jina la baba kama swala ni aibu,akasema hivi kwa nini umengangania nikamwambia mi naona kwa umri na kazi na upendo nilionao kwa watoto sina sababu ya kutoa mimba kwa sasa,akaniambia sasa sikia nikuambie nina mke ana mtoto mmoja na nategemea mwingine mwezi wa pili (huu tuliopo) na kama naendelea na msimamo wangu fine lakini hataweza kumtunza mwanangu na wala nisimtafute tena anafurahi tumejuana hawezi kuvunja ndoa yake kwahiyo ananitakia maisha mema, siku ile nilikuwa kwa rafiki yangu vinginevyo hata ningeweza kuanguaka na kuzimia kabisaa uchungu wake siwezi kuelezea kiufasaha,rafiki yangu akaniambia usitoe kaza roho mtoto utamlea tu yeye(rafiki ameolewa)
basi ukichanganya na maamuzi binafsi niliyochukua nikaamua kulea tu huu ujauzito peke yangu nimeendelea nao weee lakini huko kazini hali mbaya siitwi tena kwenye projects kama zamani yani nimechacha mpaka sasa nimetafuta kazi wee mpaka nimeishia kukubali kazi za kawaida sana hivi ninavyoongea mimba inaelekea kutimiza miezi mitano lakini honestly siko stable kifedha na baba mtoto hanibip wala kunisms.
kinachonipa hofu kuna siku nikiamka asubuhi moyo unaona nimeelemewa nakata tamaa ya kila kitu naona sitaweza naishia kulia tu lakini baadae najipa moyo ila naona kama inazidi sasa yani sina uhakika na maisha tena yani sijui hata nisemeje
ndio maana nakuomba tu ushauri maana mtoto namtaka ila haya mzingira niliyopo naona kama nitapata shida sana kuna wakati najuta sana
hebu nishauri ndugu sijui hata nifanyeje tena
natanguliza shukrani
narudia tena samahani kwa usumbufu

38 comments:

Anonymous said...

jamani dada pole sana ushuri wangu wala uctoe kaza moyo huwezi jua labda hilo ndo yai lako pekee na usisahu kumuomba mungu kila kukicha na unapoenda kulala akufungulie milango maana yeye anawea pia hata hivyo mtoto huwa niwa mama hata sisi tulio kwenye ndoa 60% unaifanya wewe mama kaza moyo na mungu akutangulie
ni mimi mama Faith

zeyttt said...

AISE POLE SANA DADA KWA MATATIZO, NDIO UKUBWA HUO, UKIAMBIWA KUWA UYAONE NDIO HAYO SASA UNAYAONA, MI KWA USHAURI WANGU WALA USITOE KABISA, KWANZA DHATI KWA MUNGU, PILI UJUI MUNGU AMEKUPANGIA NINI KWA HUYO MTOTO ANAWEZA AKAWA MSAADA MKUBWA KWAKO BAADAE HUWEZI JUA, NA IPO SIKU HUYO KAKA ATAKUJA TUU KUMFUATA MWANAE DAMU NZITO, ALAFU MI SIONI SABABU YA KUWAZA SANA MAANA UTAKACHOKULA WEWE NA YEYE ATAKULA HAWEZI KUFA NJAA HATA SIKU MOJA, NA MTOTO AKISHAZALIWA HUWA MARA NYINGI HUMLEI PEKEYAKO UTAPATA WALEZI TU NA ATAKUWA NA UKIZINGATIA UNAFANYA KAZI NA KUJIMUDU.KAZA BUTI WEWE MWANAMKE UTAKUJA KUONA FAIDA YAKE BAADAE PALE UTAKAPOKUWA NA MTOTO WAKO UNACHEZA NAYE UTASIKIA RAHA SANA ATAKUFARIJI WAKATI WA HUZUNI.

ZETTY

Anonymous said...

dada pole kwa yaliyo kupata ni kweli kabisa sometimes tunaingia kwenye matatizo na hawa wanaume weti kwa sababu wanakuwa hawasemi ukweli toka mwanzo siku zote hali huwa mbaya sana pale njia inapotaka kupatikana na hii ni mbinu ya shetani ukate tamaa na hiki kuimbe mimi nakushauri vumilia na muombe mungu wako atakusaidia maana mungu hamtupi mja wake usisahau kuomba kila siku
mama ethanjnr

Unknown said...

NDUGU YANGU UCJARIBU TENA NAKUOMBA WAZO LA KUTOA MIMBA LIONDOKE KICHWANI MWAKO, WEWE KIRI YAKUA ULIKOSA THEN UTUBIE KWA MUNGU WAKO HALAFU UMWOMBE YEYE KWANI NEEMA YAKE NI MPYA KILA IITWAPO LEO YA MUNGU MENGI HUWEZI JUA NINI KAKUANDALIA CKU ZA USONI, MTUMAINIE MUNGU SANA AKUPE MLANGO WA KUTOKEA KWANI ALISEMA JARIBU LIKIJA KWA NJIA MOJA ATAKUPA NJIA SABA ZA KUTOKEA. MAMBO YAKIENDA MRAMA SANA SHIRIKISHA NDUGU ZAKO KAMA WANAUPENDO HAWATAKUA TAYRI WAKUONE UNAANGAMIA WATAKUSAIDIA HATA KWA VIJICENT TILL UTAKAPO DELIVER THEN UTAKUA FIT KUENDELEA NA KAZI.
CHA MSINGI MSIHII SANA MUNGU AKUFUNGULIE MLANGO AMINI MUNGU ANAWEZA YOTE.
MAMA RAYN

Anonymous said...

Pole saana dada yangu,siwezi kusema najua unachopitia ila ninachojua katika haya maisha wakati wa majaribu upo kwa kila binadamu tofauti tuliyokuwa nayo ni jinsi ya kukabiliana na matatizo tuliyokuwa nayo.

Tayari unajua jema na baya na hata wakati unaandika hapa nimeona kabisa unajua ni kitu gani unastahili kufanya. Kama nia ilikuwa kutoa mimba usingepoteza muda wako kuandika hapa. Kwa hilo namshukuru Mungu.

My dear hakuna atakayeweza kukupa moyo zaidi ya Mungu! Naomba u surrender kila kitu kwake, hakuna binadamu aliyekamilika katika hii dunia ila I can tell you hata mimi naweza ku survive a day at a time by God's grace. Usimtegemee binadamu hata siku moja ni Mungu tu ndiye aliyekamilika.

Ebu kaa chini na usali, muombe Mungu mweleze yote yaliyo moyoni kama baba yako. Muombe akupe watu watakaoweza kukufariji na roho mtakatifu pia kwa ajili ya peace, patience and wisdom.

Mtoto ni baraka, kutoa mimba ni kuua. Hata wenye mamilioni kwenye account hawajui kama kesho watakua na uhai. Take a day at a time na utafika. Mimi nitakuombea bila kuchoka, usiwaze yaliyopita songa mbele dadangu!

Much love.

Anonymous said...

Nasoma machozi yanatoka yenyewe. Dada pole sanaaa na MUNGU akutangulie katika yoteeeeee wachangiaji wengine wamechangia vizuri sanaaa kiasi kwamba mwenyew nimesoma mpaka inatia moyo. Kaza moyo hayo majaribu tu na MUNGU ndo atakuongoza ila usijaribu kutoa uyo mtoto atakuja kukusaidia maisha kumbuka JIWE WALILO KATAA WAASHI LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI.

Mungu akutangulie akupe moyo wa ujasiri uone yote yanamwisho. Project utaenda labda wenzio wanakuonea huruma na tumbo uwezi kusafiri. MTUMAINI MUNGU TU

Mama Kelvin said...

Du jamani kweli baadhi ya wanaume ebu muogopeni Muumba, pole dada yangu ila nakushauri Nenda sana kwenye maombi nawe nyumbani omba sana naamini utakuwa na amani na utafalijika juu ya mimba na maisha kwa ujumla sababu naamini kila kitu kinawezekana na hakuna lisilowezekana kwa yeye atutiaye nguvu.ubarikiwe na Mungu akuongoze katika wakati huu mgumu kwako.

mama Dawood said...

Pole dear,
usiungunike moyo. Chako mama nichako... usikate tamaa. Nakumbuka nilipokua mjamzito rizki ilipotea kabisa, ijapo nipo kwende ndoa hali ilikua ngumu... Ila nilimtumaina M'Mungu akanivua salama na sasa nina kazi ya maana na namshukuru Muumba. Kuwa na subira na mrudie Mungu wako... Hakika kila amtumainie Bwana ni kama mlima wa sayuni hawata tetemeka milele daima... Mwenyezi Mungu yupo kwa ajili yetu waja wake... Kivuli chenye suuzo la roho ni Mungu wetu alie tuumba... Usijali jichanganye na ndugu, jamaa, na marafiki hutojisikia mpweke... Furahia maisha, Mungu kukapa kizazi mshukuru kwa hilo kwanza kwani wengi wanatamani wangepewa Neema hiyo...
Upate faraja na amani, uwena ujasiri... YOU WILL ACHIEVE...
WE LOVE YOU.....

Anonymous said...

dada hao woooote wanakudanganya! hamna kati yao atakayekuwepo ukiwa unataabika na huyo mtoto.
hebu usituongezee watoto wasio na baba kuishia kuwa watoto wa mtaani, we toa tu hiyo mimba.
Jiang najua utanibania comment yangu hutaiweka, ila mi naongea ukweli sio hao wengine wanaomdanganya tu, wote hao wana waume wao we utabaki unahangaika peke yako, we wafate tu!

Anonymous said...

mmm jamani we anony; unamshauri atoe mimba jamani je wewe ungetolewa jamani nasikitika kama kweli we ni mwanamke una roho hyo nasikitika sana
mama faith.

Anonymous said...

Anonymous said...

dada hao woooote wanakudanganya! hamna kati yao atakayekuwepo ukiwa unataabika na huyo mtoto.
hebu usituongezee watoto wasio na baba kuishia kuwa watoto wa mtaani, we toa tu hiyo mimba.
Jiang najua utanibania comment yangu hutaiweka, ila mi naongea ukweli sio hao wengine wanaomdanganya tu, wote hao wana waume wao we utabaki unahangaika peke yako, we wafate tu!

Thursday, March 4, 2010 3:33:00 PM GMT+03:00


lazima huyu mtu alieandika huu ujumbe ana mapepo tena mapepo mabaya,eti atoe,atoe mimba ya miezi mitano we unataka mtoto wa watu afe,we mbona mama yako hakukutoa. sikia dada mimi nina story kama ya kwako my dear na mimi mwenzio na kazi nikafukuzwagwa maana hata mwaka nilikua sijamaliza,nikaishiwa hata sent lakini nilisali sanaa na Mungu akasimama mwanangu sasa ana miaka miwili na miezi 8,mrembo na ananipa furaha na matumainiya maisha kila siku,kazi nimepata nzuri tuu na Mume vilevile Mungu kanipa...usikate tamaa kama wachangiaji wengine walivyosema mrudi Mungu na nakuahidi hatakutupa bali atakupa tumaini la milele.
Mungu akubariki na mtarajiwa mtoto wako,umeshaamua kuzaa usibadili mawazo tafadhali.

Ney

Anonymous said...

Kuna dada mmoja alitoa mimba kwa ishu inafanana na yako, baadae akapata mpenzi wa kuishi naye mpaka leo anatafuta mimba haipati huu mwaka wa kumi.Usiue kiumbe chako mungu atakulaani vibaya sana.

Anonymous said...

Mdogo wangu kulea mtoto sio lazima bwana ndio akusaidie, una ndugu na jamaa zako mtalea huyo mtoto,kuna mijibaba mingine iko kwenye ndoa na haitunzi watoto wao, kina mama wanagangamala wenyewe wewe uliye nje unafikiri baba anatunza watoto, sasa usidanganyike kusubiri boyfriend ndio atakulelea mtoto.

Anonymous said...

Kila mtoto anakuja na riziki yake

Anonymous said...

Hata mimi mimi naona huyo mchangiaji aliyemwambia huyu dada mimba ana mapepo kabisa ashindwe kwa jina la Yesu. Dada yangu mpenzi Mungu wetu anasahau dhambi na makosa yetu, tubu kwa unyenyekevu, sahau kabiasa habari za huyo mwanaume na piga goti muombe Mungu kwa uaminifu atakupa kazi nzuri, utalea mwanao na mume wa kusudi la Mungu utapewa. Ondoa hofu na kukata tamaa, tumeyapitia tunajua inavyouma lakini Mungu ni mzuri, anafariji mkimbilie tu atakusaidia.

Ubarikiwe

FM said...

Haya tena pole sana dada:Sasa kuna wanosema usitoe na wengine wanasema utoe sas swali ni kwamba hakuna hata mmoja aliyesema wewe toa mimi nitakusaidia gharama zake au wewe usitoe mimi nitakusaidia ukijifungua mtoto wako.dk

Anonymous said...

yote mmesema ila na mm nasema kilio chako mungu amesha kisikia. kula vizuri, salivizuri na lala mapema. mungu anamakusudi na maisha yako.
majaribu ni mtaji wa kuongeza imani piga goti usichoke.

Mama Collin said...

dada hao woooote wanakudanganya! hamna kati yao atakayekuwepo ukiwa unataabika na huyo mtoto.
hebu usituongezee watoto wasio na baba kuishia kuwa watoto wa mtaani, we toa tu hiyo mimba.
Jiang najua utanibania comment yangu hutaiweka, ila mi naongea ukweli sio hao wengine wanaomdanganya tu, wote hao wana waume wao we utabaki unahangaika peke yako, we wafate tu!

Naona ana mapepo huyu mchangiaji. dada usijali wala usitoe hiyo mimba jua kila jaribu lina mlango wa kutokea. mimi nilikuwa kama wewe hivyo na kazi nikasimamishwa nikamlilia Mungu kilio changu nilijifungua vema sikuamini neema ilipotokea nilipata kazi nzuri na sasa mwanangu ana mwaka na miezi tisa na ananipa faraja sana kila ninapomwona . Mungu YUKO NAWE USITOE KUUWA NA DHAMBI.

Mama Collin.

Anonymous said...

Dada nakushauri usitoe hiyo mimba japo huyo anoy hapo juu anakuambia uiotoe.

Nilipata mimba mwaka 2001 nikiwa na miaka 23 na nilikuwa mwanafunzi wa chuo nikaitoa kwa kuwa nilikuwa nasoma sikuwa na sababu yoyote nyingine.

Sasa nina miaka 31 nimeanza kutafuta mtoto tangu mwaka jana mpaka leo sijapata mimba japo madaktari wananiambia sina tatizo lolote.

Najuta kutoa ile mimba maana ningekuwa na mtoto wa miaka 8 sasa.Ushauri wangu usitoe hiyo mimba maana utakuja kujuta baadae zaidi ya unavyojuta sasa.

Kila la heri Mungu wetu ni mwema mwombe kwa imani yako atakusaidia na utubu dhambi ya kuzini nje ya ndoa.

Mungu ni mwema anasikia kilio cha kila mtu na niaamini anasikia na changu mana kila siku natubu dhambi ya kuua kiumbe kisicho na hatia maana nami mama yangu hakuniua.Wapo wanaotoa mimba kila siku na wanazipata na kutoa huyo ni shetani mkatae kabisa

Flav said...

Wamekushauri vya kutosha ila mie nakwambia nipigie kwa namba hii ni 0717-706259.mana nikukuandikia hapa haitatosha kunielewa.

Anonymous said...

My dear, wala usiumie wewe sio wa kwanza kwa hilo kila mtu anapitia mitihani ya maisha, na huo ndio mtihani wako, kama walivyosema wengine hapo juu, mtumaini Mungu hebu fikiri kama huyo bf wako angekubali mimba na mkaweka ahadi ya kuoana na kabla hamjaoana akafa je ungetoa mimba kisa kafa? jibu ni hapana ungezaa mtoto ili upate kumbukumbu yake, sasa chukulia kama amekufa, mungu akutangulie uzae mwanao na ataishi tu. MIMI NILIPATA ISHU KUBWA KULIKO HIYO DADA, NILIKUWA NA MCHUMBA AMBAYE FAMILIA ZOTE ZILIJUA, ILA SIKU MOJA KAKA YAKE ALINISHIKA KWA NGUVU WAKATI NAFANYA USAFI CHUMBANI KWANGU NA KUNIBAKA NA SIKU HIYOHIYO NILIPATA UJAUZITO, JAMBO HILI LILIENDA KWA FAMILIA NA ILISHAURIWA NIAMUE NINI CHA KUFANYA, BASI NILICHOAMUA MIMI NI KUWA SITOKAA NITOE MIMBA MAISHANI MWANGU NA MCHUMBA WANGU NINAMPENDA ILA, KWA HILI SINA BUDI KUMUACHA NA NIKAZAA MWANANGU AMBAYE BABA YAKE YUPO MPAKA LEO ILA SIHITAJI MAHUSIANO YEYOTE NA YEYE, WALA MTOTO SIJAWAHI KUMUONYESHA HUYO BABA YAKE NA SASA NI BINTI ANA MIAKA KUMI, NA NILIOLEWA NA SASA NINA WATOTO WATATU, HIVYO MAISHA YA MTU MUNGU NDIO ANAPANGA, MTUMAINI MUNGU TU.

Anonymous said...

Dada usitoe jamani utakuja kujuta mara 10 ya sasa unavyojuta, mtoto mtamu bwana huwezi jua Mungu amekupangia nini kwa hicho kiumbe, zaa dada mtoto atakua na huyo punda ipo siku atakuja kumdai. Wapo wenye ndoa na wanalea watoto peke yeo pasipo msaada wa mume sembuse wewe kwa boyfriend. Dada naomba saaaaaana usitoe huyo baby boy/girl wako.

Anonymous said...

dada akili kichwani,
umepewa nasaha nzuri sana... na nina uhakika km wasemavyo baadhi ya wadau kuwa km nia ya kutoa, ungetoa toka jana... sasa basi si wewe tu,walikuepo, wapo na watakuepo...(watoa mimba)
akili kichwani... ukitoa usijutie, ukikosa mtoto... na usipo toa usijutie msoto... ILA MUNGU YUPO...
Kazi kwako mwana blog...

Anonymous said...

Pole dada. Yaani story yako ni replay ya maisha yangu. Na mie nilikataliwa kama wewe, nikaambiwa niitoe kama sitaki tusijuane. Kusema kweli inauma, wala nisikutanie, mie nililia mpaka siku kabla sijajifungua. Kuna siku zitakua mbaya zaidi zingine zitakua nzuri. Mie nashukuru Mungu nina familia na marafiki wanaonipenda na kunijali. Ni kipindi kigumu, ukiwa na watu wanaokupenda siku zitaenda.

Mwanangu sasa ana miaka miwili, kusema ukweli ananipa faraja, nguvu na nampenda sana. Ana furaha na tunaishi maisha ya furaha. Nashukuru Mungu niliamua kuzaa kwa sababu sipati picha maisha yangu bila mwanangu.

Kama kuna kitu najutia maishani mwangu, ni kuwa mjinga na kuendelea kujipendekeza kwa huyo bwana angalau turudiane kwa sababu nilidhani itamsaidia mtoto. Nashukuru Mungu aliendelea kunikataa na sasa anaoa angalau nitaishi kwa amani na mwanangu.

Kuhusu hali ngumu, maisha si marahisi kila siku. Kama una marafiki ambao wameshazaa unaweza ukawaazima nguo za watoto kipindi ambapo bado unajiweka sana. Kuna kipindi hali itakua ngumu lakini amini usiamini mwanao atakupa nguvu hata hukujua kama unazo, utatafuta kazi kwa nguvu zote na ukirudi atakuchekea utasahau machungu yote ya siku.

Jipe moyo dada yangu, ila ukiona ni ngumu na unataka kutoa vyote ni uamuzi wako kwa sababu reality za maisha yetu zinatofautiana, ni wewe ndio unajua ukweli wa hali gani inakukabili. Kama itawezekana amua kuwa mama, utapata faraja hata kuielezea siwezi.

Anonymous said...

pole sana dada yangu. matatizo niliyonayo mm hapa ninapoandika ujumbe huu ni kama yako na tena nina mimba ya miezi 5 na bwana full mcharuko. mbaya zaidi huyu bwana nimetoka nae mbali sana since form 1 mwaka 1993 embu emagine ni miaka mingapi leo hii eti ananiambia nitoe mimba. so nimemwambia ni bora tuachane kuliko mm kuitoa hii mimba kisa kapata jimama lenye hela linamuhonga. isitoshe nimemvumilia sana kipindi hana kazi akawa anatumia zangu leo hii kapata hicho kijikazi tena kwa msaada wangu leo hii anajiona handsome boy kipindi hana kazi hao mashangingi walikuwa wapi? wanaume wote ni washenzi wa tabia na umalaya wamezoea. Kumbuka malipo ni hapahapa duniani tukaze buti tutazaa watoto wetu wazuri sana na watatupa chalenge ya maisha sana. So big up zaa mtoto ni wako. Kuna rafiki yangu mmoja anatafuta mtoto sana na sasa ana miaka 35 mpaka ameamua kwenda kuadopt mtoto kwenye vituo vya kulelea yatima. Why mm na wewe tusijivunie. Thanks God for everthing. its me mdau

Anonymous said...

Mhu! Mimi huwa napita tu humu nakuangalia picha za vimalaika zinazowekwa humu, na kufurahi na nafsi yangu.

Moja, kutoa mimba nafsi itakusuta kama inavyoendelea kukusuta ulivyotoa mara ya kwanza, utaishi na sononi hiyo maisha yako yote.

Pili uko katika wakati mgumu sana, na angelikuwa huyo mwanaume ni mume wangu ningelimlazimisha atimize wajibu wake kama mzazi, kwani kumuachia ndio anaendeleza upumbavu wake na kuumiza wanawake wengine.

Tatu inawezekana hata hao alionao kwenye ndoa hawatunzi, kwa hiyo usipate jakamoyo kwa huyo fisimaji asiyejua wajibu wake hapa duniani. Zaa mtoto wako na muombe Mungu akufungulie milango ya riziki.

Nne hapo ulipo unaona kila kitu kinaenda vibaya sababu ni mtazamo hasi ulionao sasa hivi. Sahau, safisha nafsi yako, mpuuze huyo fisi maji, nafsi yako ikikunjuka itaradiate kwenye sura yako, negativity itaondoka na utaona mambo yako na kazi vinanyooka. Concentrate on you as you as if hukuwahi kuwa na mahusiano na mtu. Hiyo positive attitude utayo iacquire itakusaidia sana na hata kujifungua kwako kutakuwa easy.

Mwisho, Jiang unaweza kufanya jambo la maana sana kwa huytu dada kwani hapo alipo ana wasi wasi na jinsi atakavyoanza maisha mapya na baby wake bila usaidizi. Unaweza ukaorganize kupitia blogu yako watu wakamfanyia VIRTUAL BABY SHOWER, ambayo si lazima yeye awepo bali mwenye kuweza kuleta vinguo vya baby, na vitu vingine vinahusiana na baby wakakuletea ukavikusanya, kisha yeye akaja kuvichukua kwako. Bahati mbaya siko Tanzania kwa sasa lakini ningelikuwepo ningelikusaidia kwa hilo. Kwa sababu kina mama walio na watoto waliopitisha zaidi ya mwaka zile nguo na vitu vingine vya mtoto mchanga havitumiki tena, na havina kazi, kwa wazungu wana system ya ku"borrow" anapewa mzazi mwingine avitumie. Mbona tunanunua za mtumba!

Sijui hilo ni wazo tu maana pengine hilo linaweza kumpa faraja zaidi akiona kuwa wanawake wengine wako pamoja na yeye kuliko kumuacha na maneno matupu tu!

Bi Mkora

Jiang said...

@Mdau hapo juu...nalifanyia kazi wazo lako, asante kwa ushauri mzuri.

mama B said...

pole sana na matatizo dada mpenzi matatizo ya hivyo yapo na sisi wengine yameshatukuta najua unavyojiskia kwa sasa ila piga moyo konde usithubutu kuitoa hiyo mimba kwasababu kilichoko tumboni hakina hatia ila ni nyinyi wazazi sioni haja ya kumuhukumu mtoto, mimi ilishanitokea na sasa nina mtoto wangu mzuri tu na usijali kuhusu huduma mungu ni mkubwa ukilea hiyo mimba hadi kujifungua utaona kila kitu kinakwenda sawa na utamfurahia mtoto wako sana tu. wanaume ndivyo walivyo hao wababa mmoja dada mungu akupe ujasiri na ikatae roho ya kishetani ya kutoa mimba.

Anonymous said...

jamani mi nina neno moja tu la kusema NASHUKURU kwa ushauri na moyo wote mlionipa,wakati nasoma comments zote machozi yamenitoka,yani nawahakikishia kuanzia leo hii nimejipanga na kubadili mtazamo kabisa,(ingawa sikuwa nafikiria kuitoa hii mimba tangu mwanzo)nitajitahidi kuomba mungu mpaka nizae mwanangu,mwenye ushauri wa ziada au kingine asisite kumuandikia jiang,nitayapokea kwa roho moja

mbarikiwe sana na mungu,
aliyeomba ushauri

Anonymous said...

mume wa mtu sumu,mtoto zaa ila atapata shida, mtoto baba na mama asikudanganye mtu, labda kwa mapenzi ya Mungu mzazi mmoja au wote waondoke duniani. Kwa kuwa maji yameshamwagika, mtoto zaa ila uanze kujitune kukubali ukweli kuwa mtoto utalea mwenyewe na usitegemee utapata msaada kwa huyo bwana. Kawaida hili ni somo sidhani kama utadanganywa tena siku nyingine. kwa wanawake tulivyo, huyo bwana anaweza kurudi baadae akakudanganya tena kwa raha za siku mbili tatu then akakujaza mimba ya pili.Mungu akutangulie kaza buti.

Unknown said...

My dear hayo yaliyokupata hata mie yalishanitokea miaka 8 iliyopita, namshukuru Mungu nilizaa salama mtoto wa kike lkn Mungu akanijaalia baada ya 4 yrs pamoja na kuzaa nikapata mchumba, nilimweleza each & everthing hatimaye tukafunga ndoa tunaishi raha mustarehe nilishasahau yote.
Mwachie Mungu na sali bila kukoma.

Lv u much.

Anonymous said...

Mama Jos' said: Pole mdogo wangu. Si unajua mume wa mtu sumu. Hata mimi mume wangu alimdanganya binti mmoja hajaoa kipindi niko mkoani kikazi. Hata nilivyofatilia na kumwambia yule dada anadanganywa hakutaka kusikia. Alimnng'ang'ania mume wangu kama luba. Matokeo yake kazalishwa na kuachwa kwenye mataa. Ninachokushauri rudi kwa mungu wako kwani huwa anajibu maombi, atakupa furaha na amani tele moyoni utasahau yote yaliyokupata na utamlea mtoto wako vizuri kwani mtoto ni zawadi toka kwa mungu. Akikua muonyeshe baba yake alipo wala usiwe na kinyongo naye kwani kwani biblia inasema unaposamehe mungu anakuponya maradhi yako yote. Usikute hata hizo project hupati sababu ya kuweka kinyongo moyoni. Take care!

Anonymous said...

nitafute dada 0772 109180 kwa ushauri zaidi,

mama Collins said...

dada.. natamani ningekuwa na uwezo ule wa kukurudisha kwenye maisha yangu ya nyuma na ya sasa..

Tupo wengi tulopitia hayo unayopitia... ni ngumu naelewa sana kuliko watu wanavyodhania...

sali kwa imani yako.. kamwe usimuache mungu kwenye hili...

Ninachojua na chenye uhakika..hili nalo litapita.. utazaa, utalea na na ukiwa una kamalaika kako mkononi.. maisha yataendelea.. na utaona the reason for you to move on na kutafuta kazi nzuri kwa ajili ya mtoto..

Believe me nikikwambia baada ya muda haya utapata kazi nzuri, na mwanao atakuwa mwenye afya tele na furaha...na utakaa kuwapa moyo ambao watakuwa wanalia kama nawe unavyolia.

Ilo limwanaume litalaaniwa.. kila chozi utoalo na limfikie... mungu hujibu hapahapa.. siku akijifanya kurudi eti namtaka mwanangu tafadhali toa humu alafu unipe nafasi ya kumshushua..

HATA HILI LITAPITA DEAR.. MWAMBIE MUNGU KILA KITU.

Anonymous said...

Pole sana dada ila ni mapenzi ya Mungu tu,kani hata mimi nimetoka huko na sasa nina mtoto mmoja ana mwaka na miezinane,hana baba kwani baba yake alimkataa akiwa bado tumboni,ila kwa sasa anajileta taratibu. Hivyo na wewe usijali iko siku mwanaume atarudi,wengi wao(Wanaume) wanogopa sana majukumu ila Mungu yupo kwani ndugu zako wapo na utashangaa utakojifungua milango itakavyofunguka.
Mama Tracy.

Anonymous said...

huyo anayekushauri utoe hiyo mimba ni ibilisi kabisaa! achana naye usifuate ushauri wake, wengi wanaotoa mimba athari yake ni kubwa sana kisaikolojia huwa hawawezi kusahau na ile damu isiyo na hatia huwa inaendelea kunena hukumu, usije ukapata hayo madhara mpendwa, Mungu atakusaidia mtumaini yeye.edna.

Carola said...

We dada acha ujinga. Toa hiyo mimba. Kwa nini unahangaika na mimba ambayo mwenzako hana time nayo?

Hawa wanaokushauri "usitoe" "usitoe" wala hawapo kukusaidia, na hawatakusaidia.

Kibebi shower sawa watakupa lakini kitakufikisha wapi?

Jenga maisha yako kwanza, kusanya pesa za project ufungue japo kamradi au vimradi vya kukustabilize kama utaamua kuzaa na mume wa mtu, au peke yako.

Hizo mimba zipo tu, na ukipata mtooaji mzuri utazichoropoa tu hata tano na bado utazaa.

Miaka 27 bado sio mzee ... kuna wenzio wana miaka 30 na hawajazaa hata mtoto mmoja hawana papara wanajijenga kwanza hata ikitokea wanalazimika kuzaa bila ndoa wamudu kulea.

Anonymous said...

The loss of fluid was a rare complication from a medical procedure, amniocentesis, in which a needle is inserted through
the woman's abdomen to withdraw a sample of amniotic fluid for genetic tests. The needle punctures the uterus and the two membranes forming the sac that holds the fetus and the fluid.

Here is my web site ... "There are * published articles and * registered authors in our article directory."